KWA ufugaji wetu wa asili, tumezowea tu kuwalisha mifugo chochote ambacho wanaweza kukipata, hususan nyasi na majani ya miti. Huo ni ufugaji wa mazowea!
Naam. Tunawapeleka ng’ombe au mbuzi mbugani au vichakani ambako wanapata lishe bora ya asili, jambo ambalo ni jema kwa sababu kadiri mifugo inapopata chakula cha aina tofauti ndivyo inavyotengeneza mseto mzuri wa nyama au maziwa.http://kijanaendelevugroup.blogspot.com/
Hata hivyo, linapokuja suala la ufugaji wakibiashara ambao una malengo ya kutengeneza kipato badala ya kufuga kwa ufahari kama tulivyozowea, ni lazima kujua namna nzuri ya kuihudumia mifugo yetu.
Ni lazima tutambue kwamba tunafuga kwa kufuata program inayoendana uzalishaji na ili kuyafikia malengo yetu ni lazima tuzingatie umakini katika kutunza mifugo hiyo.
Ndani ya MaendeleoVijijini ninazungumzia mambo mengi ya namna ya kuwahudumia mbuzi – iwe wa maziwa au nyama – maelezo ambazo yatawafaa wafugaji wote wa mbuzi bila kujali kama wanafuga kwa ajili ya maziwa au nyama.
Humu ninaelezea kuhusu namna ya wako wanapokuwa kwenye joto, namna ya kuwatunza madume, namna ya kuwatunza mbuzi kabla hawajafikia umri wa kuzaa, ukamuaji wa maziwa, , na mambo mengine mengi.http://kijanaendelevugroup.blogspot.com/
Kila kipengele kitafafanuliwa vyema ili kwa kila mfugaji wa mbuzi wa jamii mojawapo aweze kujua nini cha kufanya katika kuboresha ufugaji wake.
Ulishaji wa mbuzi
Lishe ni jambo muhimu kwa kiumbe yeyote – iwe mnyama, mdudu au mmea katika kujenga mwili na kuzaa matunda. Hivyo, ni vyema kabisa kutambua kwamba, chakula unachomlisha mbuzi wako ndicho kitakachotengeneza maziwa au nyama.
Kwa maana hiyo, ni vizuri kutambua kwamba kumpa mbuzi chakula mahali pasipo safi si jambo jema kwa sababu mbuzi hula kila aina ya chakula kwa hiyo usiwaruhusu kula chakula kilicho na mchanga. Kuwalisha chakula kilichochanganyika na mchanga kunawafanya wawe katika uwezekano mkubwa wa kupata minyoo wanaopatikana kwenye mchanga.
Unaweza kuwafungulia mbuzi wako ili wale nyasi shambani na majani ya miti vichakani, hilo ni jambo jema, hasa unapokuwa na eneo kubwa la shamba ama uko kijijini ambako maeneo ya malisho ni mengi.
Lakini mbuzi wa maziwa mara nyingi hufugiwa kwenye mabanda kwa mfumo wa ‘zero grazing’, kwa hiyo ni lazima kuwatengezea mahali pa kulia chakula na kunywea maji ambapo panahitajika kuwa juu na mbali na nyumba yao ya kulala ili wasikanyage au kuchafua chakula.
Kwa kawaida, mbuzi mwenye uzani wa wastani huhitaji takriban nusu tani au kilo 500 za chakula cha hali ya juu ama nyasi zilizokaushwa kwa mwaka huku kiwango cha kila siku kikiwa asilimia 5-7 ya uzito wake.
Kupanga chakula cha mbuzi wa maziwa ni tofauti na kupanga chakula cha paka, mbwa ama binadamu. Kama walivyo ng’ombe, mbuzi pia ni wanyama wanaocheua (ruminants). Matumbo yao yamegawanyika katika sehemu nne na wanakula nyakula vyenye asili ya mimea ambavyo vina wanga wa kutosha pamoja na maji.
Mbuzi pia wanategemea vijidudu ndani ya matumbo yao ili kumeng’enya vyakula. Hii ni sayansi ambayo kwa yeyote aliyepita darasani anaweza kuikumbuka. Wakati chakula kigumu kinapoingia kwenye sehemu ya utumbo mpana (rumen) na reticulum, wadudu jamii ya protozoa na bakteria hukimeng’enya na kukiweka katika mfumo mwingine ambao utamwezesha mbuzi kukitumia kwa ajili ya shibe, kukuza mifupa, misuli, manyoya pamoja na kutoa maziwa. Kwa namna nyingine, unawalisha wadudu, na wadudu wanamlisha mbuzi.
Hii maana yake ni kwamba mbuzi anaweza kutumia kiasi kikubwa cha chakula, hususan nyasi.
Mbuzi mzuri katika utoaji wa maziwa pia anahitaji uwezo mkubwa wa kula nyasi za kutosha. Nyasi aina ya alfalfa mara nyingi zinapendekezwa kwa ajili ya ulishaji wa mbuzi wa maziwa, kwa sababu zina wingi wa protini na madini ya kalsiumu. Hata hivyo, nyasi hizo hazipatikani kila mahali, hivyo unaweza kutumia nyasi nyingine mbadala ambazo ni laini.
Majani kama vile napier, majani ya mahindi au mtama, mboga zisizotumiwa na majani ya viazi yanapaswa kukakatwa ili kupunguza uharibifu. Pia nyasi kavu za ngano au mpunga ni chakula kizuri kwao. http://kijanaendelevugroup.blogspot.com/
Wakati wa masika unaweza kukata nyasi nyingi na kuzianika halafu uzihifadhi vizuri kwenye banda maalum ili ziwafae kwa ajili ya kiangazi ambapo nyasi huwa shida kupatikana.
Kama chakula ulichowalisha bandani kimebakia, hakikisha unakiondoa na kumbuka tu kwamba, kama mbuzi wako wanabakisha chakula kingi hii ni ishara kwamba chakula hicho ni duni, ama unawapa chakula kingi kupita kiasi, au mbuzi wako hawana hamu ya kula chakula kwa sababu wana tatizo kama vile kutojihisi vyema au minyoo.
Unaweza kuwapa mbuzi nafaka kama njia ya kubadilisha chakula tofauti na kile cha kawaida, lakini tahadhali, zoezi la kuwabadilishia chakula cha nyongeza lazima lifanyike polepole na siyo mara moja ili kuwaruhusu mbuzi kuzowea chakula kipya bila kuwadhuru. Kamwe usiwape mbuzi nafaka tupu kwa sababu zinaweza kusababisha matatizo ya tumbo.
Unaweza pia kuwalisha mbuzi wa maziwa vyakula vya maziwa vinavyolishwa na ng’ombe katika kiwango cha nusu kilo kwa mbuzi asiyekamwa, kilo moja kwa mbuzi wa kukama lita moja ya maziwa na nusu kilo kwa kila lita zaidi ya maziwa.
Hakikisha unawalisha mbuzi madini muhimu kulingana na kiwango cha maziwa wanachotoa.
Wafugaji wengi wa mbuzi hupendelea kutengeneza chakula cha nyongeza wao wenyewe ili kuokoa fedha, kukifanya chakula hicho kiwe cha asili, au kwa sababu wana nafaka nyumbani, jambo ambalo ni zuri.
Unaweza kuchanganya nafaka, lakini kamwe haiwezi kuwa gharama rahisi, na itakuwa kazi kubwa. Nafaka hizo zinatakiwa kupondwa au kusagwa katika mchanganyiko huo. Unatakiwa kuongeza kiasi cha madini na protini ili kuweka uwiano mzuri. Utakapopiga gharama ya mchanganyiko huo na muda uliotumia na vifaa itachukua muda kuviandaa, utaona bora ukanunue.
Kama unalima bustani, mabaki ya mboga mboga kama mchicha, karoti, kabichi, spinachi, sukuma wiki na nyinginezo ni muhimu kwa malisho ya mbuzi wako, lakini hakikisha umeyasafisha ili yasiwe na mchanga ambao unaweza kuwa na wadudu wengine watakaoleta madhara kwa mbuzi wako.
Jambo jingine muhimu ni kwamba, unapaswa kuwapa maji safi ya kunywa kwa wingi kama lita 5 kwa kila mbuzi wa maziwa kwa siku.
Utunzaji wa kumbukumbu
Kuweka kumbukumbu za mifugo ni muhimu katika uzalishaji kwa ajili ya kutambua kosaafu, gharama za utunzaji na faida na humsadia mfugaji kufanya uamuzi katika kuendeleza ufugaji wake.
Ikiwezekana mtumie mtaalam wa mifugo ambaye atatumia kumbukumbu hizi ili kukusaidia kuboresha ufugaji wako .http://kijanaendelevugroup.blogspot.com/
Ni muhimu sana kuweka kumbukumbu hizi:
• Kumbukumbu za idadi na ukuaji wa wanyama waliopo, jinsi zao, uzito wa kwa kila mwezi ili kufuatilia ukuaji wao, tarehe ya kuachishwa kunyonya na idadi ya waliouzwa.
• Kumbukumbu za uzazi zinazoonyesha tarehe ya kuzaliwa, namba yake, jinsi yake, aina (breed), namba ya dume/jike, na uzito wa kuzaliwa.
• Kumbukumbu za upandishaji zinazoonyesha namba ya mbuzi anayepandwa, tarehe ya joto na ya kupandwa, namba ya dume lililotumika kupanda, tarehe ya joto la pili kama atarudia na tarehe ya kuzaa.
• Kumbukumbu za chanjo na matibabu zinazoonyesha namba ya mbuzi, tarehe ya matibabu, aina ya chanjo au ugonjwa, dawa iliyotumika, idadi ya waliokufa na waliopona na jina la mtaalam aliyetibu.
• Kumbukumbu za maziwa zinazoonyesha namba ya mbuzi, tarehe ya kuzaa, kiasi cha maziwa kwa siku, na kiasi cha maziwa kwa kipindi chote cha kukamuliwa, tarehe ya kuacha kukamua na idadi ya siku alizokamuliwa.
• Kumbukumbu za mapato na matumizi zinazoonyesha mapato na matumizi, vitu vilivyouzwa au kununuliwa kwa siku, kiasi cha fedha unachokuwa nacho kila wakati, kiasi cha fedha unachodai na kudaiw
SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais kitengo cha mazingira imeweka bayana
kwamba kila jamii hapa nchini iweze kutunza na kuhifadhi mazingira ili
kurudisha mandhari ya mazingira kama yalivyokuwa kabla ya nchi ya
Tanganyika kupata uhuru wake miaka 51 iliyopita.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGg8Uoo8ksHkN050AdnZq2WRP0SEEkB0Nn0FQa5aPw4fD1HpT4kmT0j-RAqqWQYBYpoxvAOD_pO9SLE0tkDNTDnbY7_p0VK0JxfNNyUZcsW7ErAYwLx8JUdIvume1iJE52hLdL2LxJ11k/s400/Wafanyakazi+wa+TBL+wakifanya+usafi.JPG)
Kutokana na sera hiyo, kizazi cha sasa kama
kwa kufuatia historia ya hapo nyuma, hakiwezi kukubaliana kwamba katika
Ziwa Victoria kulikuwa na viumbe hali kama vile samaki wa aina mbali
mbali ambao hadi sasa baadhi yake wametoweka kabisa.
Tukichukulia mfano katika Ziwa Victoria, hapo miaka ya nyuma kabla ziwa hilo halijaingiwa na masuala ya ujangili, kulikuwa na aina mbali mbali ya samaki ambazo kwa sasa tayari ni nadra kupatikana au pengine zimetoweka kabisa.
Samaki ambazo tayari zimepotea kabisa katika ziwa Victoria kwa upande wa Tanzania ni pamoja na sangara, fulu, muru sire, sulubab na sato pamoja na aina nyingi za samaki kwa kuzitaja chache tu na kama zikipatikana na kuvuliwa katika ziwa hilo, kuna baadhi ya kizazi cha sasa cha vijana wetu hawawezi kula pengine watadai kuwa viumbe hao ni jamii ya nyoka na kwamba hawaliwi kabisa.
Lakini kwa upande wa nchi ya utafiti ambao umefanywa na taasisi ya utafiti ya Kenya Marine Research Institute unaonyesha kuwa samaki kama vile fulu, muru, sire, sulubab na samaki wengine tayari wameanza kuongezeka katika Ziwa Victoria upande wa Kenya kutokana na wananchi katika nchi hiyo kutunza na kuhifadhi mazingira ya Ziwa Victoria.
Pia utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na taasisi ya Taifa nchini Uganda ya National Fisheries Resource Research Institute (NaFIRRI) unaonyesha kuwa samaki aina ya fulu ambayo kwa lugha ya Kiganda inajulikana kwa jina na “enkejje” ambayo miaka ya sabini ilikuwa ikivuliwa kwa kuchagia kiasi cha asilimia 70 kwa idadi yote ya samaki zote zilizovuliwa miaka ya 1970 lakini hadi miaka ya 1980 uvuvi wa samaki aina ulikuwa chini ya kiwango cha asilimia kumi.
Naye Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Profesa Dkt. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed, anasema kuwa Ziwa Victoria lina umuhimu mkubwa kwa nchi zinazopata huduma kutoka ziwa hilo pamoja na nchi ya Misri ambayo inapata huduma ya maji hayo kupitia mto Nile.
Anasema kuwa katika miaka ya sitini na sabini, Tanzania ilikuwa moja ya nchi za Bonde la mto Nile zlizoshiriki kwenye mradi wa ukusanyaji wa takwimu za maji ambao ulijulikana kama Lake Victoria Hydrometric Project
Na kusema kuwa umuhimu wa Watanzania kutunza na kulinda mazingira ya Ziwa Victoria sio kwa manufaa ya nchi ya Tanzania pekee bali pia kwa manufaa ya nchi ya Misri ambayo inategemea maji kutoka Ziwa Victoria.
Anasema kuwa nchi ya Misri inanufaika kwa kiasi kikubwa katika kilimo cha umwagiliaji pamoja na shughuli zingine ambazo zinatokana na maji ambayo yanapitia mto Nile hadi Misri na shughuli hizo zinaweza zikakwamishwa endapo Watanzania hawatajikita katika kutunza na kuhifadhi mazingira ya Ziwa Victoria.
Aidha, tafiti mbali mbali ambazo zimefanywa na wataalamu wa masuala ya mazingira ya Ziwa Victoria pamoja na Bonde la Maji Kanda ya Ziwa, zinaonyesha kuwa mazalio ya samaki katika mabonde ya mito ambayo hutiririsha maji katika Ziwa Victoria nayo yamehadhiriwa vibaya na baadhi ya watu ambao hulima kando kando ya mito, kufanya shughuli za ufugaji pamoja na shughuli zingine ambazo ni athari kubwa kwa viumbe hai ambao hupatikana katika mito na maziwa.
Mratibu wa LVEMP 11, Bw Pius Mabuba anasema kwamba taasisi yake tayari imejikita katika kutatua tatizo la uchafuzi wa mazingira katika Ziwa Victoria ambao unatokana na uchafu na uharibifu wa mazingira kutoka Mto Simiyu na Duma iliyoko katika mkoa wa Simiyu.
Anasema kwamba vikundi vya kijamii vimeanzishwa kwa ajili ya kunusuru uchafuzi wa mazingira ya mito hiyo na kusema kuwa vikundi hivyo pia vitasaidia katika kuinua kipato kwa wananchi na kujiongezea uchumi katika jamii.
Vikundi hivyo vitajihusisha na upandaji miti, ujenzi wa mabwawa ya kunyweshea mifugo, kilimo ambacho ni endelevu pamoja na shughuli zingine na kuongeza kuwa katika miradi hiyo, tayari serikali kwa kushirikiana na wahisani kutoka nje imetenga sh.bilion 1,825,000,000.00 kwa ajili ya shughuli hiyo.
Anasema kuwa kamati mbali mbali ambazo zitasimamisha shughuli za utunzaji na uhifadhi mazingira ya mto Simiyu na Duma tayari zimeundwa na mikataba kati ya halmashauri husika mkoani Simiyu ambazo zitasimamia miradi hiyo imekwishasainiwa tangu Desemba 20, mwaka jana.
Naye Bw Lawrence Kalabegile ambaye pia ni mmoja wa wadau wakuu katika Mradi wa Hifadhi Mazingira ambaye katika kikao cha wenyeviti na wajumbe wa kamati za mradi wa LVEMP 11 wakati wa kikao ambacho kimefanyika katika hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza kuanzia Januari 7 hadi 9,
Anasema kwamba licha ya taasisi ya LVEMP 11 kujikita katika kusimamia shughuli za kulinda na kutunza mazingira ya Ziwa Victoria, jamii pia inao umuhimu mkubwa juu ya kujikita zaidi katika upandaji miti ili kurudisha mandhari ya nchi kama ilivyokuwa miaka hamsini iliyopita.
Anasema kuwa anaonelea hivyo kutokana na nchi ya Tanzania ambayo awali ilikuwa nchi ya “Kijani” sasa imebadirika kuwa nchi ya jangwa.
Anasema kwamba vijana wa Kitanzania wa sasa wakielezwa kuwa mkoa wa Mwanza pamoja na mikoa mingine nchini ilikuwa na miti ya asili ya kila aina, hawawezi kuelewa kwa sababu hawana historia ya uoto wa asili kwa sehemu husika hivyo wanatakiwa kufundishwa kwa nadharia na vitendo ili waweze kwenda na wakati huu ambapo dunia nzima imekumbwa na mabadiriko ya tabianchi.
Anasema kwa kulitambua hilo, timu ya Uratibu wa Mradi wa Hifadhi Mazingira ya Ziwa (LVEMP 11) wakati wa kikao chake kilichofanyika jijini Mwanza, yeye pamoja na wataalamu kutoka LVEMP 11 alionelea kuchagua shule ya Sekondari ya Lumala iliyoko katika wilaya ya Ilemela jijini Mwanza,
Iweze kusaidiwa miche ya miti zaidi ya 280 ambayo zoezi la upandaji wa miti hiyo ufanywe na wajumbe wa Kamati ya LVEMP 11 kwa kushirikiana na uongozi wa shule hiyo, zoezi ambalo limefanikiwa kwa asilimia kubwa ili kurudisha uoto wa asili katika maeneo ya shule pamoja na wanafunzi kuweza kujifunza kwa vitendo juu ya utunzaji na uhifadhi mazingira kwa kupanda miti.
Naye Bw. Christopher Mafuru ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Lumala, anasema kuwa shule yake mbali na kutoa mafunzo mengine ya kawaida, imejikita zaidi katika shughuli za uhifadhi mazingira na kwamba tayari amekuwa akisimamia shughuli za upandaji miti lakini amekuwa akikabiliwa na changamoto kadhaa ambazo zimekuwa zikikwamisha shughuli za upandaji miti katika eneo la shule.
Anasema kuwa changamoto ambazo amekuwa akikumbana nayo ni pamoja na wananchi kuchungia mifugo katika eneo la shule na baadaye miche ya miti kuharibiwa na wanyama kwa vile shule yake haina uzio wa kuzuia wanyama kuingia katika eneo la shule.
Changamoto nyingine ni pamoja na baadhi ya miche kunyauka kutokana na mizizi yake kufikia katika miamba ambako ndio ukomo wa kuendelea kuota pamoja na shule yake kutokuwa na fedha za kuendeleza shughuli za upandaji miti ambazo zinafanywa na wanafunzi wapatao 80 kutoka shuleni hapo ambao wako katika kikundi cha Mali Hai.
Naye Bw John Masota ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ambayo inajishughulisha na upandaji miti kwa lengo la kutunza na kuhifadhi mazingira ya Environmental and Conservations ya jijini Mwanza, anasema kuwa taasisi yake imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika upandaji miti katika taasisi mbali mbali za serikali pamoja na watu binafsi.
Anabainisha kuwa katika kipindi kati ya mwaka 2009 hadi 2012, taasisi yake imepanda miti aina mbali mbali ipatayo 32,000 kwa kujitolea katika maeneo ya Jeshi la Wananchi Transit Cap Nyegezi mkoani Mwanza, miche mingine 15,000 imepandwa na taasisi hiyo katika maeneo ya Gereza Kuu Butimba, miche 15,000 imepandwa katika maeneo ya Hospitali ya Wilaya ya Butimba.
Anasema kwamba taasisi yake mpaka sasa inayo miche zaidi ya 5,000 ambayo inangojea kupandwa katika maeneo mbali katika mikoa ya kanda ya ziwa kutokana na mahitaji.
Anasema kwamba taasisi yake inakabiriwa na changamoto mbali mbali hususani kutokuwa na ushirikiano mzuri na baadhi ya watendaji wa serikali ambao mara nyingi wamekuwa wakikwamisha maendeleo ya upandaji miti hususani katika wilaya za Ilemela na Nyamagana.
Lakini katika kijiji cha Sakaya, Kata ya Lubugu, wilayani Magu, kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanziia Oktoba 2011 mradi wa upandaji miti aina ya Acasia Nilotica ambao umefadhiriwa na LVEMP 11, zaidi ya hekta 32 zimepandwa miche ya miti ipatayo 1,200. Mradi huo ni mmojawapo ya miradi ya kuhifadhi dakio la mto Simiyu ambao ulivumbuliwa na wanavijiji wilayani Magu.
Katibu wa Mradi, Bw Daudi Yakobo kutoka kata ya Lubugu anasema kuwa lengo la mradi huo ni kuongeza rutuba ya udongo na upatikanaji wa miti kwa ajili ya nishati, mbao, mkaa na chakula cha mifugo na wakati huo kupunguza uharibifu wa mazingira ambao unaendelea kukumba kata hiyo pamoja na vijiji vingine wilayani Magu pia kupunguza uchafuzi wa mazingira ya Ziwa Victoria kutokana na mto huo kutiririsha maji moja kwa moja katika ziwa hilo.
Anataja uharibifu uliokuwepo ambao ni pamoja na mmomonyoko wa udongo ambao huingia kwenye vyanzo vya maji kupitia vijito vya mto Mwamaganyala na Maganzuli na hatimaye kuingia mto Simiyu kupitia mto Duma na mradi huo umegharimu sh.20,572,979.00.
Juhudi za serikali kwa kushirikiana na wananchi za kuhifadhi na kutunza mazingira kama zitakuwa endelevu, zitasaidia kutokomeza uchafuzi wa mazingira na kurudisha uoto wa asili pamoja na kunusuru viumbe hai katika ziwa Victoria ikiwa ni pamoja na samaki na wanyama na viumbe wengine na kuongeza pato la Taifa na wananchi kujikwamua kiuchumi.

Tukumbuke kuwa miti ni kitu muhimu sana katika mazingira yetu yanayo tuzunguka.Na
pia miti ni chanzo kikubwa cha maji katika mazingira yetu,Ninaweza
nikasema pia miti ndiyo kila kitu kwani miti inaumuhimu mkubwa sana
hivyo basi jamii nzima inashauriwa kutunza vyema mazingira yetu.
Tukumbuke kuwa tukikata miti ovyo tutasababisha majanga makubwa sana,kama vile kukosa vyanzo vya maji,kusababisha mmomonyoko wa udongo,

About Me
Popular Posts
-
KWA ufugaji wetu wa asili, tumezowea tu kuwalisha mifugo chochote ambacho wanaweza kukipata, hususan nyasi na majani ya miti. Huo ni ufug...
-
SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais kitengo cha mazingira imeweka bayana kwamba kila jamii hapa nchini iweze kutunza na kuhifadhi mazingira i...
-
Tukumbuke kuwa miti ni kitu muhimu sana katika mazingira yetu yanayo tuzunguka.Na pia miti ni chanzo kikubwa cha maji katika mazingira ...
Video of the day
Contributors
Powered by Blogger.